Edwin Sifuna, mgombea urais wa chama cha Equitable, amehimizwa kuzingatia zaidi azma yake ya kuwania urais badala ya kujihusisha na mazungumzo ya siri kuhusu mgombea wa muungano wa upinzani. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Herman Manyora anasema mazungumzo ya aina hiyo yanaweza kuwakatisha tamaa wafuasi ambao tayari wameunga mkono azma ya Sifuna. Hata hivyo, anabaini kuwa kugombea pekee hakuhakikishi ushindi, akionyesha kuwa hata rais aliyeko madarakani anajitahidi kuhifadhi wadhifa huo.


HERMAN MANYORA-BOARDROOM