Serikali imedhamiria kukamilisha ujenzi wa masoko ya kukusanyia na kuuzia mazao ambayo bado hayajakamilika katika Kaunti ya Kiambu. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kazi zinazoendelea katika Soko la Nyambari huko Lari, Naibu Rais Kithure Kindiki alisema Kiambu itakuwa na masoko 31 ya mazao, idadi ambayo ni miongoni mwa kubwa zaidi nchini. Alisema masoko hayo yatatoa mazingira mazuri ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wakulima.


KITHURE KINDIKI-INSPECTION