Naibu Gavana wa Kaunti ya Makueni Lucy Mulili amehimiza serikali ya kitaifa kupanua Barabara Kuu ya Nairobi-Mombasa ili kupunguza msongamano na kuzuia ajali zinazosababisha vifo mara kwa mara. Alitaja sehemu ya kuteremka yenye urefu wa kilomita tano kutoka Mlima Kiu, kati ya Kima na mji wa Salama katika kaunti Ndogo ya Mukaa. Sehemu hiyo imekuwa eneo hatai la trafiki kwa muda mrefu, ikichukua maisha ya watu wengi kupitia ajali zinazohusisha malori mazito ya kibiashara na magari ya abiria.
LUCY MULILI - KAZI