Naibu Rais Kithure Kindiki amesisitiza tena azma yake ya kuunganisha eneo la Mlima Kenya, akisema anachukulia kwa uzito mkubwa jukumu alilokabidhiwa na wazee wa eneo hilo wiki chache zilizopita. Akizungumza huko Lari, Kaunti ya Kiambu, Kindiki alisema amewasamehe wapinzani wake wa kisiasa waliomtukana na kumdhihaki. Alisisitiza kuwa ataendelea kuzingatia wajibu wake kama Naibu Rais na kuendelea kutetea maslahi ya eneo hilo na ya taifa.
KITHURE KINDIKI-UNITE