Ukatili wa nyumbani unapaswa kudhibitiwa kutokana na athari zake za kudumu kwa waathiriwa na familia. Mwanasaikolojia na mtaalamu wa ushauri wa ndoa, Susan Kahema, anasema kuwa waathiriwa wanaweza kupata kiwewe, msongo wa mawazo na mashambulizi ya hofu kali, huku watoto walioshuhudia vitendo vya ukatili wakiona tabia hiyo kuwa ya kawaida na kuirudia baadaye maishani. Anaongeza kuwa baadhi ya watoto wanaweza pia kuogopa kuanzisha mahusiano kutokana na kupitia hayo.
SUSAN KAHEMA – VIOLENCE