Kampuni ya Kenya Breweries, kupitia chapa ya Tusker, imetenga kiasi cha Shilingi milioni 14 kusaidia mashindano ya Safari Sevens ya mwaka huu, hatua inayozidi kuimarisha ahadi ya chapa hiyo kwa mchezo wa raga nchini Kenya. Kupitia ushirikiano huu, Tusker itakuwa Mshirika Rasmi wa Vinywaji vya Pombe na Burudani kwa toleo la 28 la Safari Sevens, mashindano yatakayofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11 Oktoba katika Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi. Udhamini huo utaisaidia KRU katika kuandaa mashindano hayo, pamoja na kuboresha nyanja za burudani na uzoefu wa mashabiki.
Jua linashuhudiwa Makindu, Voi na Mariakani.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.