Mombasa United iliibuka na ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya Kariobangi Sharks katika mechi ya kwanza ya mchujo wa kupanda daraja kwenda Ligi Kuu (KPL) kutoka Ligi ya NSL, iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Mbaraki, Mombasa. Dennis Toeri na Rashidi Waziri walifunga mabao hayo kwa upande wa wenyeji, huku Dalvin Wayne akiifungia Sharks bao la kufutia machozi kuelekea mwishoni mwa mechi. Mechi ya marudio itachezwa jijini Nairobi Jumanne ijayo, ambapo mshindi kwa jumla ya mabao atajihakikishia nafasi ya Ligi Kuu (KPL) msimu wa 2026/27. Kocha Mkuu wa Sharks, William Muluya, anaamini kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha mambo na kufanikiwa.

WILLIAM MULUYA- SHARKS




Jua linashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.