Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge, Dan Wanyama, ameitaka taasisi ya Sports Kenya kuandaa sera madhubuti za kibiashara na za utunzaji wa Uwanja wa Raila Odinga Talanta City baada ya mashindano ya AFCON ya mwaka 2027. Akizungumza baada ya kukagua uwanja huo, Wanyama alitangaza kuwa Kenya inaendelea vyema na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, huku akibaini kuwa ni kazi ndogo tu zilizosalia na zinatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
DAN WANYAMA - SPORTS