Wabunge wametoa wito wa kuajiriwa na kulipwa vizuri kwa Wahamasishaji wa Afya ya Jamii, wakisisitiza umuhimu wao katika kuimarisha huduma za afya ya msingi na kufanikisha ajenda ya Huduma ya Afya kwa Wote. Wabunge hao walizitaka serikali za kaunti kuboresha maslahi yao kwa kuhakikisha michango yao ya bima ya afya inalipwa na kuwapa rasilimali zinazohitajika ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Chini ya utaratibu wa sasa, wahudumu hao wa afya hupokea shilingi 5,000 kwa mwezi, ambayo hufadhiliwa kwa pamoja na serikali kuu pamoja na serikali za kaunti.


VOX POP-CHPs