Guinea Bissau iliishangaza Nigeria kwa kuichapa mabao 3-0 katika mechi ya kufuzu AFCON 2027 usiku wa jana, jambo lililoongeza shinikizo kwa kocha mkuu Eric Chele. Franculino Djú alianza kufunga katika kipindi cha kwanza kabla ya Mama Baldé na Álvaro Djaló kuongeza bao moja kila mmoja katika kipindi cha pili. Wakati huo huo, Tanzania ilitoka sare ya 1-1 na Madagascar, huku Uganda ikiifunga Libya 1-0 nayo Rwanda ikiishinda Cape Verde mabao 2-1. Matokeo mengine ya raundi ya pili yalishuhudia Mali ikiifunga Liberia bao 1-0 na Morocco ikiishinda Lesotho mabao 2-0, huku Gabon ikiifunga Niger mabao 2-0.
Kwa upande mwingine, Misri iliichapa Sudan Kusini mabao 5-0 huku Omar Marmoush akifunga mabao mawili, Ivory Coast ikiifunga Somalia mabao 2-0 na Gambia ikiishangaza Ghana kwa ushindi wa mabao 4-2. Benin iliishinda Mauritania 2-1, Comoros ikiifunga Namibia 1-0 nayo Congo ikitoka sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani, Cameroon. Msumbiji iliichapa Sudan mabao 4-1, nayo Senegal ikiifunga Ethiopia bao 1-0. Burundi ilitoka sare ya 2-2 na Algeria, huku Zambia ikiifunga Togo mabao 2-0. Ratiba ya mechi inaendelea leo ambapo Afrika Kusini itacheza dhidi ya Eritrea katika mechi ya Kundi D jijini Cairo.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.