Mabingwa wa dunia, Uhispania waliichapa Croatia 4-1 katika ligi ya mataifa ya UEFA na kudumisha nafasi ya juu katika kundi C jana usiku, huku Lamin Yamal akifunga mabao mawili. Wakati huo huo, Uingereza iliishinda Jamhuri ya Czech 2-0 kwa mabao ya Antony Gordon na Harry Kane katika kipindi cha pili, na kuwafanya Three Lions kubaki wa pili kwa pointi tatu nyuma ya Uhispania.
Matokeo mengine yalishuhudia Iceland ikiifunga Luxembourg 3-0 huku Bulgaria ikitoka sare ya 0-0 na Estonia na Slovakia ikiishinda Kazakhstan 2-1. Wakati huo huo, Uswizi iliishinda Scotland 3-0, huku Slovenia ikiishinda North Macedonia 2-0 na San Marino ikiishinda Albania 3-0.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi,
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.