Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika, Ferdinand Omanyala, amezindua klabu nyingine ya mbio fupi katika Shule ya Wavulana ya St. Joseph iliyoko Kitale. Hatua hii inakuja siku chache baada ya kuzindua klabu kama hiyo katika shule yake ya zamani, Friends School Kamusinga. Uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi pana za Omanyala za kuanzisha programu rasmi za mbio fupi shuleni na kuweka mazingira yatakayowawezesha wanariadha chipukizi kuendeleza vipaji vyao. Mshikilizi huyo wa rekodi ya Afrika ya mbio za mita 100 ana imani kuwa programu hiyo hivi karibuni itazalisha wanariadha wenye uwezo wa kufanya vizuri katika ngazi ya shule, kikanda na kimataifa.




Jua linashuhudiwa Nyeri, Nanyuki na Meru.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.