Timu ya Harambee Stars itafanya mazoezi yake ya pili jioni hii jijini Conakry, kujiandaa na mechi yao ya pili ya kufuzu kwa michuano ya AFCON ya mwaka 2027 (Kundi D) dhidi ya wenyeji Guinea kesho. Stars, ambao tayari wameshafuzu kwa michuano hiyo kama wenyeji, walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Eritrea Jumamosi, na kocha Benni McCarthy atakuwa akisaka ushindi wake wa kwanza katika kundi hilo. McCarthy anasema wanalenga kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kundi hilo huku wakijiandaa kwa michuano hiyo itakayofanyika mwakani.
Jua linashuhudiwa Gilgil, Nakuru na Nyahururu.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.