Seneti imeahirisha kikao chake hadi baadaye leo baada ya kushindwa kufikia idadi ya chini ya wabunge inayohitajika ili kuendesha shughuli za bunge. Bunge hilo lilipanga kuwahoji Mawaziri watatu kuhusu wizara zao; maaziri hao ni Waziri wa Mambo ya kigeni Musalia Mudavadi, Waziri wa Mazingira Deborah Barasa, na Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir. Angalau maseneta 15 wanahitajika ili kukidhi mahitaji ya idadi hiyo ya chini ya wajumbe.


SENATE SPEAKER-QUORUM