Chama cha Wamiliki wa Matatu kimekaribisha mpango wa kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Afrika Mashariki huko Lamu, kikisema kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kupunguza bei ya mafuta. Hata hivyo, afisa wa chama hicho, Albert Karakacha, anataka kuwekwa kwa muda maalum na wazi wa kukamilika kwa mradi huo, huku akitoa wito wa kufunguliwa kwa soko la mafuta na kufutwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA), ambayo anailaumu kwa bei ya juu ya mafuta na ongezeko la gharama za uendeshaji wa matatu.
ALBERT KARAKACHA – MATATU