Baadhi ya viongozi wa Kaunti ya Isiolo wamepongeza operesheni ya usalama inayoendelea katika sehemu za Kaunti ya Samburu, wakiielezea kuwa imechelewa kwa muda mrefu. Wakizungumza na waandishi wa habari, wakaazi kutoka jamii mbalimbali walimsihi Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen kuendeleza na kuimarisha msako ili kuondoa ujambazi na kurejesha silaha haramu na mifugo iliyoibiwa. Walionya kwamba kusimamisha operesheni hiyo kutadhoofisha juhudi za kurejesha silaha haramu na wanyama walioibiwa na kurejesha usalama kwenye mpaka wa Isiolo-Samburu.
VOX POP - ISIOLO