Kocha Mkuu wa timu ya Kenya ya vijana wa U-23, Antony Modo Kimani, anasema wako katika njia sahihi kuelekea Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles mwaka 2028, ingawa bado wana safari ndefu. Kimani aliyasema hayo baada ya ushindi wa 4-1 katika mechi ya kwanza dhidi ya Tanzania kwenye michuano ya kufuzu AFCON U-23, uliofanyika jana katika Uwanja wa Nyayo. Hata hivyo, Modo anakuwa na tahadhari kuelekea mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam wiki ijayo, huku timu kubwa ya Ivory Coast ikiwa ndiyo mpinzani wao anayefuata iwapo watafanikiwa kusonga mbele. Huyu hapa Kimani.

ANTONY KIMANI - U23



Shabiki wa soka wa Kenya amefungua kesi katika Baraza la Migogoro ya Michezo (SDT) akitaka kuilazimisha FKF na Wizara ya Michezo kulipa marupurupu ambayo bado hayajalipwa kwa timu ya Harambee Stars, ndani ya muda uliowekwa na mahakama. Brian Ngula anaomba SDT iliamuru shirikisho hilo kutoa orodha ya malipo hayo pamoja na ratiba ya lini yatalipwa. Aidha, anaomba msaada wa SDT kuilazimisha FKF na Wizara ya Michezo kuwapa wachezaji wa Harambee Stars na benchi la ufundi taarifa kamili kuhusu marupurupu hayo ambayo hayajalipwa.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.