Patrick Dorgu amerejea Manchester United kwa ajili ya tathmini baada ya kupata jeraha akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Denmark. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alitolewa uwanjani baada ya dakika 30 katika mechi ambayo Denmark iliifunga Wales mabao 2-0 kwenye michuano ya Nations League Jumapili. Alipatiwa matibabu kwa tatizo linaloshukiwa kuwa ni jeraha la misuli ya paja na amerejea Carrington kufanyiwa vipimo zaidi na madaktari wa United. Dorgu atakosa mechi ya Denmark dhidi ya Ureno pamoja na mechi ya marudiano dhidi ya Wales katika kipindi kilichosalia cha mapumziko ya mechi za kimataifa.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.