Mahakama ya Mazingira na Ardhi ya Malindi imeamuru pande zote kudumisha hali ilivyo katika eneo lenye mgogoro katika Kaunti ya Lamu hadi Oktoba tarehe 14. Hii ni huku wakaazi 133 wa Chandavai wakipinga mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote chenye thamani ya Sh trilioni 2 katika ardhi wanayodai kuwa mali ya mababu zao. Jaji Jane Onyango alikataa kuthibitisha ombi hilo kama la dharura lakini akaamuru washtakiwa wahudumiwe na kupewa siku 14 kuwasilisha majibu yao.