Timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ilifanya mazoezi yao jana katika uwanja wa Nyayo kabla ya mechi yao ya kufuzu kwa AFCON U23 dhidi ya wenyeji Kenya saa tisa mchana. Kenya ikiongozwa na kocha mkuu Antony Kimani itakuwa ikitafuta ushindi kabla ya mechi ya pili wikendi ijayo jijini Dar es Salaam. Mshindi atakabiliana na mabingwa wa Afrika Ivory Coast katika raundi ya pili, huku mechi ya bara ikiwa hatarini. Licha ya kuwakosa wachezaji muhimu kama Aldrine Kibet na Brighton Onyona Kimani ana imani watafanya vizuri.

ANTONY KIMANI - U23




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.