Waziri wa Utalii na Wanyamapori, Rebecca Miano, anasema Kenya inaweka bidhaa zake za utalii katika mfumo wa kidijitali na kuziboresha ili ziweze kupatikana kwa urahisi zaidi na wasafiri wanaotumia mifumo ya kidijitali kugundua, kupanga na kuweka nafasi za safari. Akizungumza huko Uasin Gishu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani, Waziri Miano alisema teknolojia ya kidijitali na AI zinazidi kuwa muhimu kwa ushindani wa Kenya kama kivutio cha utalii katika soko la usafiri linaloendelea kubadilika.
REBECCA MIANO – TECHNOLOGY