Leeds United waliendeleza mwanzo wao wa kutoshindwa katika kampeni ya Ligi ya Premier kwa kuichapa Newcastle mabao 4-1. Leeds walipata bao la kuongoza kupitia Lewis Miley dakika ya 32, kabla ya Jayden Bogle kuongeza la pili dakika mbili baadaye na Calvert-Lewin kufunga la tatu muda mfupi kabla ya mapumziko. Noah Okafor alifunga alifanya yawe manne dakika ya 59, kabla ya Bazoumana Touré kuwapa Magpies bao moja dakika ya 90. Matokeo hayo yaliifanya Leeds kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali wakiwa na pointi 8 nyuma ya vinara Arsenal na Manchester City.


 

Nchini Italia, Roma walidumisha nafasi ya juu katika Serie A kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Torino, kupitia juhudi za Donyell Malen na Nicolla Pisilli katika kila kipindi. Wakati huo huo, Mabingwa Inter Milan walitoka mabao mawili nyuma, na kuishinda Udinese 5-3 jana usiku. Carlos Agusto na Nicola Barella walifuta mabao ya James Abankwa na Jurgen Ekelenkamp kipindi cha kwanza, kabla ya Marcus Thuram, Pio Esposito na Ange Yoan kufunga bao katika kipindi cha pili. Inter sasa wako katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 12 sawa na Roma wakiwa na tofauti bora ya mabao baada ya mechi nne.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.