Waziri wa fedha, John Mbadi, amekanusha madai ya Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, kwamba Rais William Ruto anapanga njama ya kumfanya bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote, achukue udhibiti wa Kampuni ya Kenya Pipeline. Katika mahojiano ya televisheni, Mbadi alisisitiza kuwa uuzaji wa hisa asilimia 25 katika KPC ulikuwa makubaliano halali ya kibiashara kati ya muuzaji na mnunuzi walioridhia wenyewe. Alimtaka Nyoro kuacha kutoa kauli za kisiasa zinazoweza kuwatisha wawekezaji wa kigeni.

JOHN MBADI – SHARES