Kipa wa Senegal, Edouard Mendy, ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya miaka minane na kuichezea timu ya taifa, inayojulikana kama 'Lions of Teranga' mechi 60. Mendy, ambaye alizaliwa Ufaransa na kucheza soka ya ngazi ya juu katika klabu za Marseille, Reims na Chelsea, alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2018 chini ya kocha Aliou Cisse. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 34, anayeichezea klabu ya Al-Ahli, alitwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Misri mwaka 2021, na pia alishiriki michuano ya mwaka uliopita ambapo Senegal ilishinda bao 1–0, ingawa baadaye taji hilo lilikabidhiwa wenyeji Morocco kufuatia rufaa iliyozua utata.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.