Mwanasiasa Suleiman Shahbal ametoa wito wa kutoa elimu ya mapema kuhusu hatari za dawa za kulevya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na tatizo la matumizi ya dawa hizo katika eneo la Pwani. Mwanasiasa huyo, anayewania kiti cha ugavana katika uchaguzi wa mwaka 2027, alisema serikali za kaunti zinapaswa kuanzisha vituo zaidi vya kurekebisha tabia ili kuwasaidia wale walioathiriwa na uraibu. Akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha runinga ya NTV, Shahbal pia aliwahimiza wakaazi kutoa taarifa kuhusu walanguzi wa dawa za kulevya na kuwataka viongozi kubuni nafasi zaidi za ajira na fursa kwa vijana ili kuwaepusha na matumizi ya dawa hizo.


SULEIMAN SHABAL-CALLS