Rais William Ruto amemjibu Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kuhusu ahadi yake ya kuwagawia maafisa wa polisi nyumba za bei nafuu iwapo atachaguliwa kuwa rais mwaka wa 2027. Akizungumza jijini Kisumu, Ruto alisema serikali tayari imepanga ujenzi wa nyumba 20,000 kwa ajili ya maafisa wa polisi. Aliwataka Sifuna na upinzani kuacha kujadili mpango wa nyumba za bei nafuu, akisema hawafahamu mipango ya serikali wala maendeleo yaliyopatikana kufikia sasa.


WILLIAM RUTO-HOUSES