Rais William Ruto ameahidi kufanya kazi na viongozi wa ODM ili kuendeleza urithi wa maendeleo wa kiongozi wa zamani wa chama hicho marehemu Raila Odinga kote nchini. Akizungumza wakati wa mkutano wa mashinani na viongozi mjini Kisumu jana, Ruto alimsifu Raila kama mshauri mwenye ushawishi mkubwa katika safari yake ya kisiasa. Pia aliahidi kuimarisha ushirikiano mpana kati ya UDA na ODM, akisema ushirikiano huo utasaidia kuendeleza maendeleo kote nchini.
WILLIAM RUTO-WORK