Kurejea kwa Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kulianza kwa kuicharaza timu ya Azerbaijan Sabah mabao 4-0 jana usiku katika Uwanja wa Old Trafford. Matheus Cunha aliiweka United kifua mbele dakika ya 25 kabla ya Bruno Fernandes na Benjamin Sesko kufunga bao moja kabla ya muda wa mapumziko. Lisandro Martínez aliongeza bao la nne dakika ya 68 huku United wakiendelea kujivunia ushindi msimu huu. Wakati huo huo, Bayern Munich walianza kampeni yao kwa ushindi mzuri wa mabao 5-0 dhidi ya Bodo Glimt kwa bao la Michael Olise.


Mechi zingine zilishuhudia Como ikiichapa Lepzig 4-1, huku Fernebahce ikitoka sare ya 1-1 na Roma, na Slavia Praha ikipoteza 3-2 dhidi ya Lens. PSV ilikamilisha mechi za siku ya kwanza kwa sare ya 1-1 na Shakhtar Donesk.




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.