Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi, Silas Obuhatsa, amewataka wakuu wa shule na Bodi za Usimamizi kutathmini hali ya shule zao na kuweka mikakati ya kuwalinda wanafunzi dhidi ya mvua ya El Niño. Anasema wazazi wanapaswa kuhakikishiwa usalama wa watoto wao, huku akisisitiza kuwa shule hazipaswi kufungwa mapema kutokana na mvua hiyo. Obuhatsa anabaini kuwa uzoefu uliopatikana kutokana na mafuriko ya hapo awali unapaswa kuziongoza shule katika kujiandaa kwa dharura zinazoweza kujitokeza.


SILAS OBUHATSA –EL NIÑO