Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ameishutumu hadharani serikali ya Rais William Ruto kwa kuwasumbua na kuwahangaisha wawekezaji huku ikitumia nyadhifa zake kuendeleza maslahi ya kibiashara binafsi. Kiongozi huyo wa chama cha People's Party alitaja kampuni ya Tata Chemicals Magadi kama mfano wa mwekezaji wa kigeni aliyetumiwa ilani ya kuondoka nchini bila haki. Badala yake, aliitaka serikali kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayovutia wawekezaji zaidi nchini Kenya.


NDINDI NYORO - NAFASI