Kesi inayomkabili aliyekuwa Waziri Raphael Tuju, kuhusiana na madai ya kutoa taarifa za uongo kuhusu tukio linalodaiwa kuwa la utekaji nyara, imechukua mkondo mpya baada ya afisa wa polisi aliyepokea malalamiko yake, kueleza mahakamani kuwa aliingiwa na hofu baada ya kugundua jina lake limejumuishwa katika hati ya mashtaka. Mkaguzi Mkuu wa Polisi Purity Kobia, ambaye wakati huo alikuwa akihudumu katika Kituo cha Polisi cha Karen, aliambia mahakama kuwa hakuelewa ni kwa nini jina lake liliwekwa kwenye hati hiyo ya mashtaka.


 VOX POP – OFFICER