Kenya bado haijabaini iwapo visa vya kujitoa uhai nchini vinapungua kutokana na kukosekana kwa mfumo wa kitaifa wa kuorodhesha matukio hayo. Daktari wa magonjwa ya akili Linnet Ongeri anasema kuwa takwimu kuhusu kujiua bado hazijajumuishwa pamoja licha ya kuwepo kwa makadirio, jambo linalofanya iwe vigumu kupima maendeleo yaliyopatikana. Kenya ilikuwa imeweka lengo la kupunguza visa vya kujiua kwa asilimia 10 kufikia mwaka wa 2026 kupitia Mkakati wake wa Kitaifa wa Kuzuia Kujiua, lakini maendeleo hayo bado hayajathibitishwa.


LINNET ONGERI – REGISTRY