Baraza la Dini Mbalimbali, kwa ushirikiano na Wizara ya Afya pamoja na Cambridge, limezindua mwongozo wa kuwasaidia viongozi wa dini kushughulikia visa vya kujitoa uhai. Daktari wa magonjwa ya akili Linnet Ongeri anasema mwongozo huo utawaelekeza viongozi wa dini jinsi ya kutoa msaada, kushughulikia hali hiyo kwa huruma, na kuwaelekeza walioathirika kupata huduma za kitaalamu. Anasema pia unalenga kupunguza unyanyapaa, akibaini kuwa watu wengi walionusurika kujitoa uhai hupata changamoto katika kutafuta msaada kwa sababu suala la kujitoa uhai bado linachukuliwa kuwa mwiko.


LINNET ONGERI – HANDBOOK