Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itawekeza Shilingi bilioni 1 kukarabati upya Uwanja wa Kericho Green, ambao uliandaa sherehe za Siku ya Mashujaa za mwaka 2023. Ruto alisema uwanja huo ulikarabatiwa kwa haraka ili kuandaa hafla hiyo ya kitaifa na haukukidhi viwango vinavyohitajika. Akizungumza mjini Kericho, Rais pia alitangaza mipango ya kujenga uwanja wa kisasa huko Kapkret na hospitali ya rufaa huko Kipkelion, huku ujenzi ukitarajiwa kuanza mwezi ujao.


WILLIAM RUTO-STADIUM