Kamati kuu ya Utendaji ya Kitaifa ya FKF inatarajiwa kukutana wiki ijayo ili kuidhinisha marekebisho ya sheria za 2019 kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya FKF wa 2026/27. Hii inafuatia mkutano wa jana kati ya Wakurugenzi Wakuu wa Klabu za FKF na KPL, ambapo ilikubaliwa kwamba ligi hiyo itachezwa chini ya kanuni za mwaka 2019, kulingana na agizo la mahakama. Hata hivyo, marekebisho kadhaa yatafanywa ikiwa ni pamoja na ongezeko lililopendekezwa la mgao wa wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi saba kwa kila klabu.
Klabu za KPL zinapanga mashindano ya kabla ya msimu ili kunoa vikosi vyao kabla ya kampeni mpya, ambayo tarehe yake ya kuanza bado haijulikani kutokana na migogoro inayoendelea mahakamani. Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka KPL na NSL, na kuzipa klabu maandalizi muhimu ya mechi huku zikisubiri ufafanuzi kuhusu mechi ya ufunguzi wa msimu. Mgogoro wa kisheria wa Kariobangi Sharks na FKF umepangwa kurejea katika Mahakama Kuu ya Milimani kwa maelekezo zaidi tarehe 21 mwezi huu, huku rufaa ya msingi ikiwekwa siku tatu baadaye.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.
Ili ku[ata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.