Timu ya wavulana ya Kenya ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 15 lazima iwashinde wenyeji Rwanda kwa njia ya kushawishi, ili kufuzu kwa nusu fainali ya Mashindano ya Soka ya Shule za Afrika ya CAF yanayoendelea jijini Kigali. Hii inakuja baada ya kupoteza kwao 4-0 dhidi ya Tanzania, ikifuatiwa na sare ya 0-0 dhidi ya Sudan katika kundi A jana. Katika kundi la wasichana, Kenya iliwalazimisha mabingwa Tanzania sare ya 0-0 na kubaki wa tatu katika kundi B, wakiwa na pointi moja. Tanzania ambayo iliwashinda Somalia 5-0 inaongoza jedwali kwa pointi 4. Wakati huo huo, Somalia ambayo iliwashinda Sudan 5-0 ni ya pili kwa pointi tatu.


FIFA imeishutumu  inayshirikisho la kusimamia soka barani Ulaya, UEFA kwa kuanzisha kampeni ya kashfa dhidi ya Gianni Infantino katika changamoto ya hatua za kisheria kuhusu jaribio lililoshindwa la kuuza sehemu ya Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi. UEFA imewasilisha kesi za kisheria katika mahakama za Marekani ikitafuta ushahidi unaohusiana na mradi huo wenye utata na kuonya kuwa inafikiria kuanzisha kesi za jinai dhidi ya Infantino nchini Uswizi. UEFA inajaribu kumtoa Infantino madarakani kwa kujiuzulu au katika uchaguzi wa rais wa FIFA mwezi Machi.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kitale,Kisii na Kericho.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.