Pyramids FC wanatarajiwa kuwasili Nairobi jioni ya leo, kabla ya mechi yao ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF dhidi ya Gor Mahia. Timu hiyo ya Misri itafanya mazoezi katika uwanja wa Police Sacco kwa siku mbili kabla ya kucheza katika uwanja wa Nyayo Jumamosi, siku moja kabla ya mechi mechi hiyo. Washindi hao wa ligi ya mabingwa ya mwaka 2024 wanaanza kama wanaopigiwa upatu, huku Ko'gallo wakitarajia kuwaangusha katika mkondo wa marudiano uliopangwa wiki moja baadaye jijini Cairo.


Malkia Strikers watakuwa wakitafuta kusogea karibu na taji lao la 11 la ubingwa wa Voliboli ya Wanawake ya Afrika kwa kuwashinda wapinzani wao Cameroon katika nusu fainali jioni hii. Malkia, walishinda Algeria 3-1 katika robo fainali Jumanne na watakuwa wakitafuta ushindi kwa nafasi katika fainali, huku michuano ya dunia na nafasi ya Olimpiki ya Los Angeles ya 2028 ziking'ang'aniwa. Mechi hiyo inaanza saa moja usiku, huku Misri ikipambana na Rwanda katika nusu fainali ya kwanza saa kumi jioni. Kocha mkuu wa Malkia Geoffrey Omondi ana uhakika wa ushindi.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Nakuru.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.