Timu ya Kenya ya wavulana walio chini ya umri wa miaka 15 imepangwa katika Kundi A, katika mechi za kufuzu za CECAFA za CAF za Soka ya Shule za Afrika mwaka 2026 jijini Kigali, Rwanda. Kenya itapambana na wenyeji Rwanda, Sudan na Tanzania, huku Uganda ikikabiliana na Somalia, Sudan Kusini na Burundi katika kundi B. Kulingana na droo iliyofanyika jana, Wasichana wa Kenya walio chini ya umri wa miaka 15 watapambana na Tanzania Sudan na Somalia katika kundi B, huku wenyeji Rwanda wakicheza dhidi ya Burundi, Sudan Kusini na Uganda katika kundi A. Kocha mkuu wa timu ya wavulana Patrick Nyale ana imani watafanya vizuri.
Mshambuliaji wa zamani wa Kariobangi Sharks Masoud Juma amejiunga rasmi na mabingwa wa Ligi Kuu ya Jordan, Al Hussein SC. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, wa Harambee Stars anajiunga na miamba hao wa Jordan kama mchezaji huru kufuatia kuondoka kwake kutoka klabu ya Lebanon Al Nejmeh SC mwezi uliopita. Tangu aanze kazi yake ya kitaaluma na Shabana mwaka 2014, Juma amechezea vilabu 15, huku hatua yake ya hivi karibuni ikiongeza sura nyingine katika kazi ambayo imempeleka kote Kenya, Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Kakamega na Eldoret.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.