Klabu ya AS Roma imewasilisha ofa yao ya kwanza kwa Chelsea kumsajili mshambuliaji Alejandro Garnacho.
Ofa hiyo ni ya mkopo wenye ada ya pauni milioni 4.3 pamoja na kipengele cha kumnunua kwa pauni milioni 30, ambacho kitakuwa cha lazima endapo masharti fulani yatatimizwa.
Hata hivyo, Chelsea wanadaiwa kuhitaji pauni milioni 50 ili kumuuza nyota huyo.
…………………
Paris Saint-Germain wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo ya kumsajili Lucas Digne kutoka Aston Villa mara baada ya Kombe la Dunia.
PSG wanatarajiwa kulipa pauni milioni 8.5 kwa beki huyo wa kushoto, ambaye yuko tayari kurejea katika klabu yake ya zamani.
Hata hivyo, uhamisho huo utasubiri hadi amalize majukumu yake na timu ya taifa ya Ufaransa, ambayo itavaana na Uhispania katika nusu fainali.