Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, wanamfuatilia mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Ferran Torres, kama mbadala wa Bradley Barcola iwapo winga huyo ataondoka klabuni.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ufaransa, Liverpool wanaendelea kuwania sahihi ya Barcola, huku PSG wakianza maandalizi ya kuziba pengo litakalotokea endapo uhamisho huo utakamilika.

…………………

Newcastle United wamepoteza kiungo wa Freiburg, Johan Manzambi, ambaye sasa anatarajiwa kujiunga na Aston Villa.

Inadaiwa nyota huyo wa Uswisi ameipa Villa kipaumbele baada ya klabu hiyo kukubali kufikia dau la pauni milioni 49 ambalo Newcastle walikuwa wamekubaliana na Freiburg.

Fursa ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya imeelezwa kuwa sababu kuu ya uamuzi wake. Manzambi alikuwa amekubaliana masharti binafsi na Newcastle, lakini alisubiri kumaliza kampeni ya Kombe la Dunia kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Uswisi iliondolewa na Argentina kwa mabao 3-1 katika robo fainali.