Sekta ya mashirika ya kijamii hapa nchini imepongezwa kwa kuchangia zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika mali na kupanua huduma za kifedha kwa mamilioni ya Wakenya.
Hata hivyo, wadau wanasema changamoto kubwa zinazoikabili sekta hiyo ni uongozi dhaifu, udanganyifu na mifumo duni ya usimamizi.
Haya yanajiri huku bunge la kitaifa likijiandaa kujadili miswada mipya ya Vyama vya Ushirika inayolenga kuimarisha uwajibikaji, usimamizi na kuendana na mabadiliko ya huduma za kifedha za kidijitali.
……………………
Bunge la Kitaifa linatarajiwa kupata mamlaka zaidi ya kusimamia fedha za umma zinazopelekwa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki iwapo Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Benki hiyo wa mwaka 2026 utapitishwa.
Mswada huo, unaodhaminiwa na Kiongozi wa Wengi Kimani Ichung’wah, unapendekeza Hazina ya Taifa ipate idhini ya Bunge kabla ya kuidhinisha au kutoa fedha kutoka Hazina Kuu kwenda benki hiyo ya kikanda.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma.