Hali ya ongezeko la ukosefu wa usalama shuleni imewaacha walimu wengi wakihofia usalama wao wanapotekeleza majukumu yao.

Mtaalamu wa elimu Joel Tondokori anasema visa vinavyoongezeka vya walimu kushambuliwa vinatatiza shughuli za masomo na kuathiri utendaji kazi darasani.

Anaitaka serikali, wasimamizi wa shule na wazazi kuimarisha usalama shuleni, huku akisitiza hoja ya nidhamu na kukuza heshima kwa walimu katika taasisi za elimu.

JOEL TONDOKORI – TEACHERS