Klabu ya Manchester United inatarajiwa kukamilisha usajili wa Andrey SantosnaKarl Darlow hii leo.Wachezaji hao wote wawili wamefaulu vipimo vya afya na wamekubaliana masharti ya kibinafsi na klabu hiyo.
Wawili hao wanatarajiwa kufika Carrington hii leo kutia saini mikataba yao huku United ikijiandaa kurejea rasmi kwenye mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wiki ijayo.
Wakati uo huo, vipimo vya kina vya afya kwa kiungo Ederson bado vinaendelea, huku United wakitarajia kukamilisha usajili wake katika siku chache zijazo.
…………………
Klabu ya Newcastle United imekubaliana masharti ya kibinafsi na Johan Manzambi na pia wamefikia makubaliano na Freiburg kuhusu uhamisho wenye thamani ya pauni milioni 49.
Hata hivyo, Manzambi hatatia saini mkataba hadi atakapomaliza kushiriki Kombe la Dunia, ambako ameifikisha Uswisi hatua ya robo fainali.
Newcastle wanaamini pia kuwa kuna klabu nyingine bado zinamwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.
Ingawa Newcastle wana matumaini makubaliano yatakamilika, bado wanaendelea kuwa waangalifu baada ya kushuhudia Victor Munoz akichagua kujiunga na Liverpool dakika za mwisho mwezi uliopita.