Nahodha wa Newcastle United, Bruno Guimarães, ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kujiunga na Arsenal.

Newcastle hawajatoa kauli yoyote kuhusu suala hilo, huku ikisemekana kuwa Arsenal bado hawajawasiliana rasmi na klabu hiyo kuhusu upatikanaji wa kiungo huyo wa kati.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa masharti ya uwezekano wa uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yamejadiliwa kupitia kwa wapatanishi.

Guimarães amesalia na miaka miwili kwenye mkataba wake na Newcastle, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja hadi majira ya kiangazi ya mwaka 2029.

Newcastle hawana nia ya kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, na msimamo wao umekuwa wazi tangu mwanzo wa dirisha la usajili kuwa nahodha wao hauzwi na hawapokei ofa zozote.

……………….

Klabu ya Manchester United inatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji Marcus Rashford kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

United wanataka kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kabla ya kuelekea kambini kwa  maandalizi ya msimu mpya yatakayofanyika mjini Dublin mwezi ujao.

Hata hivyo, inaripotiwa kuwa klabu hiyo ina mpango wa kumrejesha Rashford kwenye kikosi cha kwanza baada ya Barcelona kuamua kutotumia kipengele cha kumnunua mchezaji huyo kufuatia kipindi chake cha mkopo kukamilika.