Klabu ya Manchester United imekubaliana na Chelsea kumsajili kiungo Andrey Santos kwa ada ya pauni milioni 50.
Makubaliano hayo yanajumuisha pauni milioni 48 zilizohakikishwa pamoja na pauni milioni mbili kama nyongeza kulingana na mafanikio.
Chelsea pia watabaki na asilimia 10 ya fedha za mauzo ya baadaye ya mchezaji huyo.
Santos sasa anajiandaa kufanyiwa vipimo vya afya na Manchester United.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikabiliwa na ushindani mkubwa wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara msimu huu kutokana na Chelsea kutoshiriki mashindano ya bara Ulaya na ndoto yake ya kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza ilizidi kuwa ngumu baada ya Moises Caicedo kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2033 mapema mwaka huu.
Santos alijiunga na Chelsea akitokea Vasco da Gama, na baadaye akacheza kwa mkopo katika Nottingham Forest na na kisha klabu dada ya Chelsea, Strasbourg.
Msimu uliopita alicheza mechi 43 katika mashindano yote akiwa na Chelsea, huku akifunga mabao matatu na kutoa pasi nne za mabao.
………………
Kiungo wa kati Aurélien Tchouaméni, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Real Madrid, licha yaje kumezewa mate na klabu ya Manchester United.
Inaarifiwa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa juu ya orodha ya Manchester United.
Hata hivyo, Tchouaméni sasa anaonekana kuwa tayari kuendelea na maisha yake katika Real Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kusalia katika uwanja wa Santiago Bernabéu.