Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, amemtaka Rais William Ruto kuacha kuwatukana viongozi wa upinzani pindi wanapodai uwajibikaji kutoka kwa serikali yake. Sifuna anasema upinzani hautashiriki katika siasa za matusi, huku akiahidi kuwa viongozi wa 'Linda Mwananchi' watadumisha nidhamu na kujikita katika siasa zinazozingatia hoja, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
EDWIN SIFUNA – MATUSI