Nitawashinda washindani wangu katika uchaguzi wa 2027 iwe wataungana au watagombea urais tofauti, Rais William Ruto ametangaza. Akizungumza wakati wa ziara ya maendeleo katika kaunti za Elgeyo-Marakwet na Baringo, Ruto alisema wakosoaji wake walikuwa wakipoteza muda wao kwa kuwa na wasiwasi jinsi ya kuungana, akisema watashindwa uchaguzi ujao kwa vyovyote vile. Aliwaelezea wapinzani wake kama wafanyabiashara wa hasira, chuki na ubaguzi ambao hawana cha kuwapa Wakenya.

WILLIAM RUTO - UNGANA