Naibu Gavana wa Kakamega Ayub Savula ameitaka Wizara ya Afya kuanzisha vituo vya uchunguzi wa Ebola kwenye korido za usafiri wa malori za masafa marefu. Savula ametoa wito wa uchunguzi wa kina wa madereva wanaoingia nchini, hasa wale wanaowasili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo imeripoti mkurupuko. Pia alizitaka serikali za kaunti na kitaifa kushirikiana katika kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.


AYUB SAVULA-EBOLA