Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula amewasihi wakaazi walioko kwenye mpaka wa Kenya na Uganda kuendelea kuwa macho kufuatia uthibitisho wa kisa cha kwanza cha Ebola nchini Kenya. Akizungumza huko Bungoma Wetang'ula aliwasihi wakaazi kufuata miongozo ya Wizara ya Afya na kuendelea kuwa macho. Gavana wa Bungoma Ken Lusaka alisema utawala wake umeanzisha hatua za kuimarisha ufuatiliaji na uchunguzi wa watu wanaovuka mpaka ili kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.


MOSES WETANGULA-EBOLA