Wakulima wa chai katika Zone 3 ya Murang'a wanatishia kuachana na kilimo cha chai kwa ajili ya mazao mbadala kufuatia malipo ya chini ya bonasi ikilinganishwa na wenzao katika Zone 2. Wakulima walipokea Shilingi 30 kwa kila kilo dhidi ya KSh47 zilizolipwa katika Zone 2. Mbunge wa eneo hilo Peter Kihungi amemtaka Gavana Irungu Kang'ata kuunda kikosi kazi cha kuchunguza tofauti hiyo, huku akimhimiza DCI kuchunguza madai ya ukiukwaji wa sheria katika ununuzi wa mbolea wakati wa mwaka wa fedha wa 2024/25.
VOX POP-TEA